Dodoma FM
Dodoma FM
5 December 2025, 4:11 pm

Aidha ameongeza kuwa hali hiyo inawalizimu kusafiri kilomita kadhaa kwenda vituo vya afya vya kata jirani ili kupata vipimo zaidi.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa kukosekana kwa maabara katika zahanati ya Igandu Wilaya ya Chamwino imepelekea baadhi ya wananchi kupewa matibabu kulingana na maelezo yao jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Akizungumzia changamoto hiyo Mwenyekiti wa Kijiji Cha Igandu Bi.Joyce Chiloweka amesema licha ya uwepo wa zahanati kijijini hapo lakini wagonjwa hawanufaiki na vipimo pindi wanapofika kupata huduma za afya.
Chiloweka amesema kuwa wagonjwa wamekuwa wakitibiwa kulingana na maelezo ya mgonjwa jambo ambalo halina uhakika wa asilimia mia moja juu ya anachotibiwa.
Nao baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Masamaki wamesema hali hiyo ya kukosa uhakika wa matibabu inawalizimu kusafiri kufuata huduma bora japo huleta mashaka kwa wamama wajawazito na watoto wachanga.