Dodoma FM
Dodoma FM
4 December 2025, 3:44 pm

Kwa mujibu wa Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS), kiwango cha udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kimeshuka kutoka asilimia 34 mwaka 2015 hadi wastani wa asilimia 30 mwaka 2022.
Na Yussuph Hassan.
Wanawake wameshauriwa kuzingatia lishe hasa kabla ya miezi 3 ya kubeba ujauzito ili kujifungua salama.
Wito huo umetolewa na Afisa Lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Bi Vailet Mrema wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema lishe bora kabla na baada ya ujauzito itaamua afya ya mtoto atayezaliwa.
Bi Vailet amesema mama anayetarajia kupata ujauzito akizingatia lishe bora kabla na baada ya ujauzito inasaidia kutengeneza afya ya motto hivyo jamii haina budi kuzingatia suala hilo.