Dodoma FM

Uhaba wa maji wachochea migogoro ya ndoa Manchali

3 December 2025, 3:51 pm

Changamoto ya maji imekuwa ikiwaathiri zaidi wanawake kwani hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji. Picha na Nukta Habari.

Wanawake hao wameongeza kuwa wanaporudi nyumbani hukumbana na ugomvi pamoja na wivu kutoka kwa wenza wao.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Manchali walalamikia kutembea umbali mrefu kutafuta maji hali inayopelekea migogoro ya ndoa ya mara kwa mara kijijini hapo.

Wakazi hao wamesema ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara hulazimika kuwatuma watoto kutafuta maji mbali hali inayohatarisha usalama wa watoto .

Sauti za wakazi.

Manyangalazi Manyangalazi  ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Manchali amesema kuwa kijiji hicho kilichimbiwa kisima ambacho maji yake ni ya chumvi sana hayafai kwa matumizi ya nyumbani hali inayopelekea wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta maji safi na salama.

Amesema wamesubiri muda mrefu ahadi ya Shirika la Innovation of Africa kuja kuwachimbia kisima kijijini hapo lakini bado hakuna utekelezaji wowote hadi sasa.

Sauti ya Manyangalazi Manyangalazi.

Katika uzinduzi wa sera ya Taifa ya maji ya mwaka 2002 toleo la mwaka  2025 serikali ilisema imelenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji ili kufikia lengo la asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini ifikapo Desemba 2025 ambapo kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji ni asilimia 83 vijijini na asilimia 91 mijini.