Dodoma FM
Dodoma FM
3 December 2025, 3:28 pm

Licha ya uokotaji taka kuwa chanzo cha kipato kwao, mchango wao katika kuweka mazingira katika hali ya usafi umeendelea kutambuliwa na wadau wa mazingira. Picha na Google.
Hatua nyingine ni kuhakikisha waokota taka wanapatiwa vitambulisho rasmi vitakavyowatambua na kutambua kazi wanayoifanya katika jamii.
Na Lilian Leopold.
Waokota taka rejeshi jijini Dodoma wametajwa kuwa miongoni mwa nguzo muhimu katika kulinda mazingira, huku juhudi zikiendelea kuhakikisha wanakuwa na elimu na vifaa vya kujikinga kutokana na mazingira hatarishi wanayo fanyia kazi.
Wakizungumza na Taswira ya habari Afisa mazingira kutoka Kampuni ya Mazingira ya Tongyi Queen Mwita pamoja na Msimamizi na Afisa Masoko wa Shirika la Juza Waste Pickers Inititive Jemma Frank wamesema wanaendelea kutoa elimu na msaada wa vifaa kinga kama vile reflector, viatu vigumu na glovu ili kuwakinga na madhara wanayoweza kuyapata kutokana na mazingira hatarishi ya kazi.
Aidha, wameeleza mikakati mingine ni kuanzisha vituo vidogo vya ununuzi wa taka ili kupunguza umbali mrefu ambao waokota taka hulamizika kutembea na kuuza taka wanazokusanya.

Tanzania inakadiriwa kuzalisha kati ya tani milioni 14.4 na milioni 20.7 za taka ngumu kwa mwaka, ikiwa ni wastani wa kilo 241 hadi 347 kwa mtu mmoja kwa mwaka na kuongeza kuwa maeneo ya mijini yanakadiriwa kuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji taka ikilinganishwa na vijijini.