Dodoma FM

Maafisa usafirishaji watakiwa kuzingatia elimu matumizi vyombo vya moto

3 December 2025, 4:24 pm

Ukosefu wa elimu ya uendeshaji wa vyombo vya moto kwa baadhi ya madereva bodaboda pomoja na baadhi ya madereva kujihusisha na uhalifu.Picha na mtandao.

Amewataka vijana kujitahidi kupata elimu na uelewa wa jinsi kuendesha vyombo vya moto pamoja na kufahamu sheria zza barabarani kala ya kuingia barabarani kuendesha vyombo hivyo.

Na Daniel Njau.

Maafisa usafirishaji almaarufu kama Bodaboda Jijini Dodoma wametakiwa kuzingatia kanuni za usafirishaji pamoja na elimu ya matumizi ya vyombo vya moto ili kulinda usalama wao na wa abiria.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa maafisa usafirishaji Mkoa wa Dodoma Bw. Chacha Marwa ambapo amesema kumekuwa na ongezeko la vijana wanaomaliza vyuo na kujiingiza moja kwa moja katika udereva bodaboda ili kujipatia kipato .

Sauti ya Bw. Chacha Marwa

Aidha ameeleza changamoto wanazo kutana nazo ni pamoja na uwepo wa vituo vya bodaboda na bajaji visivyo sajiliwa, ukosefu wa elimu ya uendeshaji wa vyombo vya moto kwa baadhi ya madereva bodaboda pomoja na baadhi ya madereva kujihusisha na uhalifu ukiwemo wizi na uporaji.

Sauti ya Bw. Chacha Marwa

Kwa mujibu wa Takwimu ya  idadi ya bodaboda na bajaji eneo la Dodoma mjini ni takribani Bajaji 17000, bodaboda 6000 huku idadi ya boda boda kwa mkoa mzima ikiwa ni 24000.