Dodoma FM

Serikali kuwashirikisha vijana katika mipango ya maendeleo

1 December 2025, 4:27 pm

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimtunuku mhitimu wa ngazi ya Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Salome Njau, katika mahafali ya 39 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Duru ya Kwanza, Kampasi Kuu – Dodoma..Picha na Chuo cha Mipango.

Sheria ya Ununuzi wa Umma imeelekeza taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya manunuzi yote kwa ajili ya makundi maalumu wakiwemo vijana ili kuongeza ushiriki wao katika uchumi wa Taifa,

Na Anwary Shaban.
Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuwaamini vijana na kuwashirikisha kikamilifu katika mipango mbalimbali ya maendeleo ya uchumi, ikiwa ni dhamira ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuchangia kwa ufanisi katika ustawi wa Taifa.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar kwenye mahafali ya 39 ya Chuo cha Mipango na  Maendeleo Vijijini, na kuwataka kuchamkia fursa zilizopo.

Sauti ya Mhandisi Mshamu Ali Munde.

‎Aidha Mkuu wa chuo hicho Profesa Hozen Mayaya  amesema namna ambavyo serikali inawawezesha vijana  kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya  mahitaji soko la dunia. 

Sauti ya Profesa Hozen Mayaya.

‎Kwa upande wa wahitimu wamezungumza namna walivyojiandaa kuchangamkia fursa hizo kwa bidii.

Sauti za wahitimu.

Sheria ya Ununuzi wa Umma imeelekeza taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya manunuzi yote kwa ajili ya makundi maalumu wakiwemo vijana ili kuongeza ushiriki wao katika uchumi wa Taifa, kukuza ujasiriamali na kupunguza ukosefu wa ajira.

Aidha, serikali imeanzisha madirisha maalumu ya uwekezaji kwa vijana, kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana kupata mikopo nafuu, mitaji ya uwekezaji, mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha, ushauri wa kitaalamu na huduma za kukuza biashara