Dodoma FM

Vijana waimarisha usalama mtaani kupitia mikutano ya mitaa

1 December 2025, 1:01 pm

Picha ni ofisi ya Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma inayopatikana kata ya Miyuji mtaa wa Mailimbili. Picha na Lilian Leopold.

Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha Tanzania ina zaidi ya vijana milioni 21.3 kati ya watu milioni 61, sawa na zaidi ya theluthi moja ya idadi ya watu.

Na Lilian Leopold.

Ushiriki wa vijana katika mikutano ya mitaa ni muhimu kwa kuwawezesha  kufahamu fursa zilizopo kwenye jamii na kupata nafasi ya kuwasilisha changamoto zinazowahusu moja kwa moja.

Leo tunakuletea simulizi ya kijana Yunusi Malapula kutoka kata ya Majengo mtaa wa Fatina. Yunusi ni miongoni mwa vijana waliochochea wazo la kuimarisha ulinzi shirikishi katika mtaa wake kufuatia kuwepo kwa matukio ya kihalifu katika mtaa huo.

Kupitia ushiriki wake katika mikutano ya mtaa na kuhamasisha wenzake, Yunusi ameonyesha namna ambavyo vijana wanaweza kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto za kiusalama katika maeneo yao.

Sauti ya masimulizi na Lilian Leopold.