Dodoma FM
Dodoma FM
28 November 2025, 3:31 pm

Ukosefu wa umeme katika kijiji hicho umekuwa ukiathiri shughuli zao, kwani hulazimika kwenda kijiji cha jirani kupata huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya mashine kwa ajili ya kusaga unga.
Na Farashuu Abdallah.
Wananchi wa kijiji cha Pandambili A wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakabiliwa na adha ya umeme ambayo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu, adha hii inawalazimu kwenda maeneo ya jirani kupata huduma za kijamii.
Taswira ya habari imezungumza na wananchi hao, ambapo wamesema ukosefu wa umeme katika kijiji hicho umekuwa ukiathiri shughuli zao, kwani hulazimika kwenda kijiji cha jirani kupata huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya mashine kwa ajili ya kusaga unga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Pandambili A Bw.Remmy Chimotoro amewasihi wananchi kuwa na subra wakati serikali ikiendelea na juhudi za kutatua changamoto hiyo.