Dodoma FM
Dodoma FM
28 November 2025, 2:18 pm

Ni vyema wananchi wakachangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo fursa ya mikopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Na Mariam Matundu.
Wananchi wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Wito huo umetolewa tarehe 27 Novemba na Naibu waziri wa wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalumu Mh.Mhandisi .Maryprisca Mahundi katika kikao cha kuangazia fursa na vikundi vya malezi na matunzo ya watoto kata ya Ihumwa jijini Dodoma.
Waziri Mahundi amesema ni vyema wananchi wakachangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo fursa ya mikopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Aidha Mh.Naibu Waziri amewasihi wazazi wawe na tabia ya kuwashirikisha watoto katika kazi za kiuchumi ili kujenga kizazi kizuri chenye uwajibikaji.
Nao baadhi ya wanavikundi wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha katika fursa mbalimbalina kuwapa elimu ya malezi bora kwa watoto.