Dodoma FM
Dodoma FM
27 November 2025, 3:53 pm

Itakumbukwa kuwa Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kote duniani.
Na Seleman Kodima.
Halmashauri ya Chamwino imezindua kampeni na kutoa elimu kuelekea maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani, katika Kijiji cha Mjelo, Kata ya Handali.
Elimu hiyo imetolewa na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Chamwino, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania, TAWJA.
Bi. Penina Manyanki, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewahimiza pia wazazi kuona umuhimu wa kupeleka watoto shule ili kupata elimu, akibainisha kuwa elimu ni nyenzo muhimu ya kupunguza ukatili na unyanyasaji katika familia na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mratibu wa TAWJA Kanda ya Kati, Mheshimiwa Jaji Juliana Mvungi, amesisitiza umuhimu wa watoto wa kike kujiamini na kujikomboa kielimu na kiuchumi ili kupambana na ukatili wa kijinsia, ambao mara nyingi huwakumba zaidi wao.
Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yameendelea kuhimiza mshikamano wa jamii katika kupinga vitendo vya ukatili, huku viongozi na wadau wakisisitiza kuwa elimu na mshirikiano wa jamii ni silaha muhimu ya kupunguza tatizo hilo.