Dodoma FM
Dodoma FM
26 November 2025, 3:12 pm

Ikumbukwe kuwa Kupitia bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025/26, Serikali imepanga kuimarisha miradi ya maji vijijini, kujenga mabwawa mapya, na kuongeza uwezo wa miundombinu ya maji ili kukidhi ongezeko la watu na kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Na Farashuu Abdallah.
Tukisalia kwenye Sekta ya Maji,Imeelezwa kuwa wakazi wa Kijiji cha Pandambili, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maji, Serikali inalenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama kwa umbali usiozidi mita 400 kutoka makazi yake hali ambayo ni tofauti na katika kijiji cha Pandambili.
Aidha Wananchi wa kijiji hicho wamesema ukosefu wa maji umekuwa ukiathiri majukumu yao ya kila siku na kuwalazimu kutembea umbali mrefu kufuata maji katika vijiji jirani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Pandambili, Bw. Remmy Chimotoro, amewataka wananchi kuwa na subira wakati huu ambapo Serikali inaendelea na mikakati ya kutatua changamoto hiyo.