Dodoma FM
Dodoma FM
25 November 2025, 1:19 pm

Hata hivyo chanjo ni ngao ya kwanza ya afya ya mtoto na ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Serikali ya kulinda maisha ya wananchi wake.
Na Mariam Kasawa.
Imeelezwa kuwa mtoto anapozaliwa kinga yake ya mwili huwa ni ndogo sana, hivyo anahitaji chanjo ambazo zitamkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Hapa nchini Tanzania, tangu chanjo za awali zilipoanza kutolewa kikamilifu, zimechangia kupunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa na vifo vya watoto.
Midwife Anitha Mganga anaeleza kwa nini chanjo za awali ni muhimu sana kwa mtoto na magonjwa yanayozuilika kupitia chanjo hizo.
Anitha anasema chanjo ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuwaweka watoto kwenye afya bora.
Pia zinawalinda dhidi ya magonjwa hatari na yanayoweza kutishia maisha kama vile surua, polio na homa ya ini.
Kwa mujibu wa Sera ya Afya ya Taifa, Serikali imeweka kipaumbele cha kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo stahiki kwa wakati, ili kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuimarisha afya ya jamii.
Kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo (EPI), Tanzania imefanikiwa kuongeza kiwango cha chanjo kwa watoto, hatua ambayo imepunguza milipuko ya magonjwa na kuimarisha kinga ya jamii.
idha, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa afya wa ndani na kimataifa kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa uhakika na kwa gharama nafuu.