Dodoma FM

‘Wazazi, walezi wana jukumu kubwa malezi ya watoto’

24 November 2025, 3:37 pm

Watoto wanapopokea adhabu zisizo na maana, hujifunza kwamba hisia zao hazina umuhimu.Picha na AI.

Wazazi wasiozungumza na watoto wao au kuwanyima nafasi ya kueleza mawazo na hisia, huwafanya watoto kushindwa kueleza matatizo yao.

Na Joseph Julius.
Wazazi wanatajwa kuwa na jukumu kubwa katika malezi ya watoto, lakini tabia zisizo sahihi zinaweza kuathiri saikolojia ya mtoto na kusababisha madhara ya muda mfupi na mrefu.

Mwanasaikolojia wa maendeleo ya watoto, Dkt. Neema Winson Kimambo, amesema baadhi ya tabia za wazazi zinaweza kuharibu ustawi wa akili na hisia za mtoto.

Sauti ya Dkt. Neema

Dkt. Kimambo ameongeza kuwa watoto wanapopokea adhabu zisizo na maana, hujifunza kwamba hisia zao hazina umuhimu, jambo linaloweza kuathiri ujasiri wao wa kimaisha.

Aidha, amesema watoto wanahitaji upendo, mwongozo na usikilizaji kutoka kwa wazazi.
Ameonya kuwa wazazi wasiozungumza na watoto wao au kuwanyima nafasi ya kueleza mawazo na hisia, huwafanya watoto kushindwa kueleza matatizo yao, hali inayoweza kusababisha chuki na kuvurugika kihisia.

Dkt. Kimambo amesema wazazi wanapokuwa wavivu kuweka mipaka au kuwachukulia watoto bila sheria thabiti, watoto hufanya maamuzi mabaya kwa hila au upungufu wa hila, hali inayosababisha ukosefu wa nidhamu na changamoto za kijamii.