Dodoma FM
Dodoma FM
24 November 2025, 3:17 pm

Tangu kutangazwa kuwa jiji mwaka 2016, Dodoma imeongozwa na Mameya wawili, Jafari Mwanyemba na Profesa Davis Mwamfupe, ambaye pia amechukua fomu kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Na Mwandishi wetu.
Jumla ya makada 19 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu za kuomba kugombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya wa Jiji la Dodoma.
Akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari, Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Wilaya ya Dodoma, Amani Mlagizi, amesema kati ya wagombea hao, madiwani tisa wamechukua fomu za kuwania nafasi ya Meya na madiwani 10 nafasi ya Naibu Meya, ambapo wanawake ni wawili.
Mlagizi amesema wagombea wote 19 tayari wamerejesha fomu zao na mchakato sasa umeingia katika vikao vya ngazi ya mkoa kwa ajili ya mapendekezo ya majina yatakayowasilishwa kwenye hatua inayofuata.
Ameongeza kuwa baada ya vikao hivyo kukamilika, tarehe ya uchaguzi itatangazwa ili kupata viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.