Dodoma FM

Serikali yatumia mkakati huu kuboresha huduma ya maji Dodoma

24 November 2025, 2:57 pm

Picha ni Waziri wa Maji Juma Aweso wakati Akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).Picha na DUWASA.

Wizara itatoa kipaumbele katika kuimarisha huduma kwa wateja ili kupunguza kero na malalamiko ya wananchi.

Na Selemani Kodima
Serikali kupitia Wizara ya Maji imeanza kutekeleza mkakati maalum wa kuboresha huduma ya maji katika Jiji la Dodoma kwa miradi ya muda mfupi yenye thamani ya shilingi bilioni 62.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji Juma aweso wakati Akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA),ambapo amesema wizara itatoa kipaumbele katika kuimarisha huduma kwa wateja ili kupunguza kero na malalamiko ya wananchi. Amesisitiza kuwa huduma zinazotolewa lazima ziwe bora, za kuaminika na endelevu kwa kuzingatia Mkataba wa Huduma kwa Mteja.

Sauti ya Waziri wa Maji Juma Aweso.

Kwa upande wa uzalishaji, Waziri Aweso ameielekeza menejimenti ya DUWASA kuongeza kiwango cha uzalishaji maji kutoka lita milioni 88 kwa siku hadi kufikia lita milioni 121 kwa siku.

Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.Picha na DUWASA.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, aliwataka watumishi wa DUWASA kuzingatia nidhamu kazini, kutumia lugha sahihi kwa wateja na kushughulikia changamoto za wananchi kwa ufanisi.

Sauti ya Mhandisi Mwajuma Waziri.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, amewakumbusha watumishi wa mamlaka hiyo kutambua wajibu wao ili kufanikisha lengo la kuwahudumia wakazi wa Dodoma.

Sauti ya Mhandisi Aron Joseph.