Dodoma FM
Dodoma FM
24 November 2025, 2:16 pm

Pamoja na hayo maafisa lishe wamehimiza jamii, walimu na wazazi kushirikiana na vituo vya afya na shule katika kuunga mkono juhudi za elimu ya lishe, ili kuhakikisha watoto wanapata afya bora, akili timamu na mwili wenye nguvu tangu siku za awali za maisha yao.
Na Lilian Leopold.
Wanawake wajawazito wametakiwa kuzingatia makundi sita ya chakula wakati wa ujauzito ili kuimarisha afya zao, kukuza mwili na ubongo wa mtoto.
Wito huo umetolewa na Maafisa Lishe, Warda Sakii kutoka Kituo cha Afya Ilazo na Frida Mollel kutoka Kituo cha Afya Makole, wakati wa kutoa elimu ya afya na lishe katika Kata ya Kizota jijini Dodoma. Tukio hilo limehusisha walimu, wanafunzi na wananchi.
Maafisa lishe hao wamesema makundi hayo sita ya chakula ni pamoja na………
Aidha, wamesisitiza umuhimu wa mama mjamzito kuhudhuria kliniki mara tu anapojua kuwa ana ujauzito ili kupata elimu sahihi kuhusu makuzi na afya ya mtoto.
Kwa upande wake, Hamida Mkingule, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kizota, amesema shule hiyo inazingatia lishe kwa wanafunzi wake kwa kutoa uji na chakula chenye virutubisho.