Dodoma FM

Zifahamu Fursa za Teknolojia zinazoweza kuwaingizia vijana kipato

21 November 2025, 3:18 pm

Zaidi ya asilimia 45 ya vijana nchini wanatumia mitandao ya kijamii na teknolojia ya kidijitali kama chanzo cha kipato.Picha na AI.

Iwapo vijana watawezeshwa na kupata mafunzo ya teknolojia, zaidi ya asilimia 60 wanaweza kuingia rasmi kwenye ajira za kidijitali.

Na Seleman Kodima.
Imeelezwa kuwa zipo fursa nyingi zinazoweza kupatikana kupitia teknolojia na kusaidia vijana kujiingizia kipato.

Katika mjadala uliofanywa na mwandishi wetu Selemani Kodima, baadhi ya vijana wamesema kuwa zaidi ya asilimia 45 ya vijana nchini wanatumia mitandao ya kijamii na teknolojia ya kidijitali kama chanzo cha kipato, ikiwemo biashara mtandaoni na huduma za kidijitali.

Majadiliano.

Kwa upande wake, mtaalamu wa TEHAMA kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Sayansi ya Kompyuta Dodoma, amesema kuwa iwapo vijana watawezeshwa na kupata mafunzo ya teknolojia, zaidi ya asilimia 60 wanaweza kuingia rasmi kwenye ajira za kidijitali na kuchangia pato la taifa.