Dodoma FM
Dodoma FM
21 November 2025, 1:38 pm

Daraja hilo limekuwa kero kwa wakazi hao na kuathiri shughuli zao za kila siku.
Na Farashuu Abdallah.
Wakazi wa mtaa wa Goima, wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, wameiomba Serikali kukarabati daraja lililodhoofika na kuwa kero kubwa hususan msimu wa masika.
Wakizungumza na Dodoma FM, wakazi hao wamesema daraja hilo limekuwa likisababisha madhara kwa wananchi na kuathiri shughuli za kila siku.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mtaa wa Goima, Sapar Ramadhani Nyati, amesema yupo kwenye jitihada za kushirikiana na Serikali ili kukarabati daraja hilo na kuondoa adha inayowakabili wananchi.