Dodoma FM
Dodoma FM
21 November 2025, 1:02 pm

Wiki ya Lishe inasisitiza kuwa jukumu la kuhakikisha watoto wanapata lishe bora ni la jamii nzima—kuanzia wazazi, walezi hadi taasisi za malezi ya watoto.
Na Anwary Shaban.
Wiki ya Lishe imeendelea kuadhimishwa nchini, huku wataalam wakisisitiza umuhimu wa lishe bora kwa watoto.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 30 ya watoto chini ya miaka mitano wanakabiliwa na udumavu, na zaidi ya milioni 3.2 wapo hatarini kukosa virutubisho muhimu.
Frida Molel, Afisa Lishe kutoka Dodoma, amesema lengo kubwa la Wiki ya Lishe ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu lishe sahihi, hasa kwa watoto wadogo.
Aidha, Molel amewataka wazazi kuhakikisha watoto wanapata chakula kutoka makundi yote sita ya lishe, akisisitiza lishe kamili huchangia afya ya mwili na akili.
Kwa upande wake, Rehema Andrew, Mkurugenzi wa Tehla Day Care, amesema kituo chake kimekuwa kikitoa vyakula vyenye protini na wanga ili kujenga miili imara kwa watoto.
Naye Justa Zanaki,ni muuguzi kutoka Zahanati ya Mpama, amesema wamekuwa wakitoa elimu ya lishe kwa wazazi na kufuatilia afya za watoto mara kwa mara.