Dodoma FM

Dodoma jiji yaendelea kujinoa kuelekea ligi kuu Tanzania bara

20 November 2025, 4:13 pm

Picha ni baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Dodoma jiji.Picha na Dodoma jiji fc.

Msemaji wa Kikosi cha Dodoma jiji Fc Moses Mpunga ameeleza juu ya maandalizi hayo.

Kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ambapo Dodoma jiji itacheza na Namungo Fc wameendelea kujinoa ili kufanya vizuri katika mchezo huo.

Akiongea na Taswira ya habari Msemaji wa timu ya Dodoma jiji Fc amesema wanaamini kupitia mchezo huu wa tarehe 21 watakwenda kupata alama nzuri ili waweze kujisogeza kwenye msimamo wa ligi kwa kupata alama tatu.

Sauti ya michezo.