Dodoma FM
Dodoma FM
20 November 2025, 3:46 pm

Wameiomba mamlaka husika kuwasaidia kujaza kifusi kinachoweza kustahimili msimu wa mvua .
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kijiji cha Mpwayungu, wilaya ya Chamwino wameeleza matesowanayo pitia kufuatia ubovu wa barabara hali inayo kwamisha shughuli zao.
Wamesema kuwa ubovu huo wa miundombinu ya barabara imekuwa ni changamoto kwa vyombo vya usafiri pamoja na wasafiri jambo ambalo hugeuka mateso kwa akina mama na hata watoto pindi wanapohitaji kutumia barabara hiyo kufuata huduma na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mwenyekiti wa kijiji Mpwayungu Ndg.Festo Manjechi amekiri uwepo wa changamoto ya ubovu wa barabara ndani ya Kijiji chake na kuomba mamlaka husika kuwasaidia kujaza kifusi kinachoweza kustahimili msimu wa mvua .