Dodoma FM
Dodoma FM
20 November 2025, 3:20 pm

Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria ya PPRA, taasisi za serikali zinatakiwa kutenga asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi wa umma kwa ajili ya makundi maalum ya wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.
Na Seleman Kodima.
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma – PPRA, imesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA, katika masuala yasiyo ya ununuzi wa umma.
Hatua hii inalenga kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ajira na kushirikisha wananchi wengi zaidi katika sekta ya ununuzi wa umma.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa PPRA, Denis Simba, amesema ushirikiano huo ni muhimu kwa kuwa utasaidia kuhakikisha makundi mbalimbali ya wananchi yanashiriki kikamilifu katika ununuzi wa umma kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kuwa kwa sasa kuna vikundi zaidi ya elfu moja vilivyosajiliwa kwenye mfumo wa Nest, huku akisisitiza lengo ni kufikia vikundi elfu ishirini katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa VETA, CPA Antony Kasore, amesema makubaliano hayo yatasaidia kuviwezesha makundi maalum kupata ujuzi na mafunzo ya ufundi stadi, ili waweze kujiajiri au kuajiri wengine na hivyo kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi.