Dodoma FM

Serikali yatakiwa kuingilia kati mgogoro wa Ardhi Bwawani

20 November 2025, 1:38 pm

Migogoro ya ardhi imekuwa ikisababisha baadhi y wananchi kuvunjiwa nyumba zao bila taarifa.Picha na AI.

Mwenyekiti amewataka wananchi, pindi linapotokea jambo, kukaa pamoja na kufanya maridhiano badala ya kuchukua uamuzi unaoweza kuleta athari kwa wananchi wengine.

Na Farashuu Abdallah.
Wananchi wa Mtaa wa Bwawani kata ya Mkonze jijini Dodoma wameiomba serikali iwasaidie kutatua mgogoro wa ardhi uliopo katika mtaa huo.

Wakizungumza na Dodoma Fm baadhi ya wananchi hao wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro huo, wakisema kuwa migogoro ya ardhi imekuwa ikisababisha baadhi y wananchi kuvunjiwa nyumba zao bila taarifa.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Bwawani Sospeter Abeli amewataka wananchi kuwa watulivu, huku akiiomba serikai kutoa ufafanuzi juu ya suala la uvunjifu wa nyumba za baadhi ya wananchi.

Sauti ya Sospeter Abeli .