Dodoma FM

Baba ruksa kumwona mtoto hata kama hatoi matunzo

19 November 2025, 1:55 pm

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto namba 13 ya mwaka 2023.Picha na AI.

Wakili Jacquiline amesisitiza endapo baba anakataa au anashindwa kutoa matunzo, mama anaweza kufika ofisi za Ustawi wa Jamii au kufungua kesi mahakamani, ambapo mahakama inaweza kuamuru baba kugharamia chakula, elimu, afya na makazi ya mtoto kulingana na kipato chake.

Na Lilian Leopold.
Imeelezwa kuwa baba ana haki ya kumwona mtoto wake hata pale anaposhindwa kutoa matunzo.
kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto namba 13 ya mwaka 2023, ambayo inalenga kulinda maslahi ya mtoto juu ya tofauti za wazazi.

Wakili Jacquiline Geoffrey Mutahangarwa kutoka Ofisi ya Wakili ya Competens International Attorneys jijini Dodoma amesema mzazi wa kiume hataondolewa haki hiyo kwa sababu ya kutokutoa matumizi.

Sauti ya Wakili Jacquiline Geoffrey.

Amefafanua kuwa mazingira pekee yanayoweza kumnyima baba haki ya kumwona mtoto ni yale yanayohatarisha usalama wa mtoto, ikiwemo kusudi la kumdhuru.

Sauti ya Wakili Jacquiline Geoffrey.

Baadhi ya wazazi kutoka kata ya Majengo jijini Dodoma wamesema ni jukumu la wazazi kuhakikisha tofauti zao binafsi haziingilii haki na ustawi wa mtoto.

Sauti za wazazi.