Dodoma FM

Watakiwa kutumia fursa za kiafya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza

17 November 2025, 4:07 pm

Jamii imekuwa ikikabiliwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na mazingira wanayoishi.Picha na AI.

Wito huo umetolewa na Bi. Florian Kazi, mwakilishi wa shirika la External International kutoka China, linalojihusisha na utoaji tiba kwa magonjwa sugu bila upasuaji, katika semina fupi iliyofanyika kanisa la Mt. Joseph, Ihumwa jijini Dodoma.

Na Victor Chigwada.
Wananchi wametakiwa kutumia fursa za kiafya zinazotolewa na mashirika binafsi pindi yanapotembelea maeneo yao, ili kujikinga na magonjwa sugu na yasiyoambukizwa.

Bi. Kazi amesema jamii imekuwa ikikabiliwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na mazingira wanayoishi, hivyo ni vyema wakazi wa Ihumwa kutumia uwepo wa shirika hilo kufanya vipimo na kupata tiba mapema.

Sauti ya Bi. Florian Kazi

Aidha, ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, yapo magonjwa yanayotokana na mionzi ya jua kwa ngozi ya binadamu, hivyo kuhudhuria semina mbalimbali za afya kutasaidia kujenga uelewa na kuimarisha afya bora.

Sauti ya Bi. Florian Kazi

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema wamepata uelewa wa namna ya kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa na wametoa wito kwa jamii kufuata ushauri wa wataalamu wa afya ili kujikinga na magonjwa hayo.

Sauti za washiriki.