Dodoma FM

BMH kuanzisha kliniki ya kidonda kisukari

14 November 2025, 4:50 pm

Tatizo la kisukari kwa Jamii limeshuka huku zaidi ya asilimia 70 ya wananchi hawatambui kama wanaishi na Ugonjwa wa kisukari.Picha na BMH.

Wananchi wamehimizwa kula vyakula vya kulinda mwili na  kuachana na tabia bwete ya kukaa bila mazoezi.

Na Mariam Kasawa.
Hospitali ya Benjamin Mkapa inatarajia kuanzisha kliniki ya Kidonda kisukari ili kuwasaidia wagonjwa wa kisukari kupata huduma hiyo kwa ukaribu.

Kila Novemba 14 ni siku ya kisukari Duniani siku hii imetumika kutoa elimu pamoja na kuwataka Wananchi kuzingatia lishe ambayo haina sukari nyingi na kufanya mazoezi na kutumia bogaboga nyingi ili kuweza kujikinga na haya matatizo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof. Abel Makubi ameyabainsha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma amesema kliniki hiyo itasaidia wagonjwa wa kisukari ambao hupata shida ya mguu kupata kidonda.

Makubi ameyabainsha hayo wakati akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.Picha na BMH.

Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Omary Ubuguyu  amesema Tatizo la kisukari kwa Jamii limeshuka huku zaidi ya asilimia 70 ya wananchi hawatambui kama wanaishi na Ugonjwa wa kisukari.

Dkt Ahmed Makwani Mkurungezi kutoka Wizara ya afya ameahimiza wananchi kula vyakula vya kulinda mwilina  kuachana na maisha bwete ya kukaa bila mazoezi.

 Wakati dunia inaadhimisha leo siku ya kisukari Takwimu zilizotolewa na WHO Mwaka 2022  kanda ya Afrika zinaonyesha kiwango cha changamoto ya ugonjwa wa kisukari Afrika ni kikubwa ambapo watu wazima milioni 24 wanaishi na ugonjwa wa kisukari na idadi inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 129% hadi kufikia watu million 55 ifikapo mwaka 2045.