Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwa karibu na watu wanaopitia changamoto

14 November 2025, 4:23 pm

Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kujitenga pindi wanapokumbwa na changamoto.

Wananchi hao wamesema ni muhimu watu kutoogopa kueleza changamoto wanazopitia ili kupata msaada mapema, badala ya kuamua kujifungia ndani na kuendelea kuteseka kimya kimya

Na Farashuu Abdallah.
Katika juhudi za kukabiliana na vifo vinavyotokana na changamoto za afya ya akili, jamii imetakiwa kuwa karibu na watu wanaopitia matatizo mbalimbali yanayoweza kusababisha madhara makubwa kiafya.

Wito huo umetolewa na Mfamasia kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, kitengo cha utegemezi na uraibu wa dawa za kulevya, Steward Laison.

Akizungumza na Dodoma FM, Laison amesema ni vyema jamii ichukue hatua kwa watu wanaoonesha kukata tamaa ya maisha kwa kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma ili waweze kupatiwa matibabu mapema.

Sauti ya Steward Laison.

Ameongeza kuwa endapo mtu hatapatiwa matibabu ya haraka, madhara makubwa yanaweza kujitokeza, ikiwemo kujiua au kuathirika zaidi kiakili.

Aidha, ametoa ushauri kwa jamii kuacha tabia ya kujitenga pindi wanapokumbwa na changamoto, badala yake washirikiane na kupata msaada wa kitaalamu.

Sauti ya Steward Laison.

baadhi ya wananchi wamezishauri mamlaka mbalimbali kutoa elimu ya afya ya akili kwa jamii ili kuepusha madhara yanayoweza kuathiri mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Sauti wananchi.