Dodoma FM

Ringo Iringo kuboresha miundombinu ya barabara Miyuji

14 November 2025, 3:14 pm

Wananchi wa Kata ya Miyuji wanapaswa kutarajia mabadiliko makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.Picha na AI.

Ameongeza kuwa ahadi alizotoa wakati wa kampeni zitakuwa kipaumbele chake, hususan katika kuboresha barabara za mitaa ambazo zimekuwa kero kwa muda mrefu.

Na Seleman Kodima.
Baada ya kupata ushindi wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Miyuji kwa kura zaidi ya elfu 16, sawa na zaidi ya asilimia 92 ya kura zote 16,800, Diwani mteule wa kata hiyo, Ringi Iringo, amewahakikishia wananchi kuwa ataanza mara moja kushughulikia changamoto za miundombinu ya barabara za mitaa pindi atakapoapishwa rasmi.

Akizungumza kwa njia ya simu katika mahojiano maalum, Iringo ambaye ni mara yake ya kwanza kushika nafasi ya uongozi, amesema wananchi wa Kata ya Miyuji wanapaswa kutarajia mabadiliko makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Sauti ya Mh. Ringi Iringo,