Dodoma FM
Dodoma FM
14 November 2025, 2:15 pm

Sambamba na hayo, Jerome Marando ametoa wito kwa jamii nzima, hususan maafisa usafirishaji, kuendelea kujitokeza bila hofu kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.
Na Anwary Shaban.
Imeelezwa kuwa kundi la maafisa usafirishaji maarufu Bodaboda limekuwa mstari wa mbele kujitokeza kuchangia damu hali ambayo ni tofauti na makundi mengine.
Hatua inakuja ikiwa Shirika la afya Duniani limewahi kubainisha kuwa Tanzania inahitaji takribani chupa 550,000 za damu salama kwa mwaka ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa.
Aidha Makundi yanayohitaji damu zaidi: Wagonjwa wa upasuaji, akina mama wajawazito, watoto wenye upungufu wa damu, na waathirika wa ajali ndio hutumia damu kwa kiwango kikubwa
Taswira ya habari tumefanya mahojiano na Mratibu wa Damu Salama Jiji la Dodoma, Jerome Elson Marando, amesema mwitikio wa jamii umefikia asilimia 85.
Hata hivyo, Marando ametaja changamoto zinazowakabili maafisa hao, ikiwemo kupoteza muda mrefu wakisubiri huduma ya uchangiaji.
Amesema mifumo imeendelea kuboreshwa ili kuokoa muda na kuhakikisha huduma zinapatikana kwa haraka.
Baadhi ya maafisa usafirishaji wa jiji la Dodoma wameomba kuongezewa elimu ya kutosha kuhusu uchangiaji damu.