Dodoma FM
Dodoma FM
12 November 2025, 1:53 pm

Aidha Wakazi wa Ukalanzila wameendelea kuomba msaada wa haraka ili kuondokana na changamoto hiyo, wakisisitiza kuwa upatikanaji wa maji safi ni msingi wa afya na maendeleo ya jamii.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kitongoji cha Ukalanzila, kilichopo katika Kata ya Muungano, Wilaya ya Chamwino, wameeleza namna wanavyoathirika na matumizi ya maji yasiyo safi na salama kutokana na ukosefu wa huduma ya maji katika eneo lao.
Wakizungumza na taswira ya Habari, baadhi ya wakazi hao wamesema kuwa tangu awali walizoea kutumia maji ya visima vya asili bila kuathiriwa na magonjwa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mzula, Kenneth Msanjila, ambaye kijiji chake kinajumuisha kitongoji cha Ukalanzila, amesema kuwa wamekuwa wakifanya jitihadi mbalimbali za kuboresha huduma ya maji.
Miongoni mwa hatua wanazochukua ni kutafuta wafadhili watakaosaidia kusogeza huduma ya maji safi kwa wakazi wa Ukalanzila.
Kwa upande wake, Diwani mteule wa Kata ya Muungano, Msafiri Atanasi, amekiri kuwepo kwa mapungufu ya huduma ya maji katika baadhi ya vitongoji, ikiwemo Ukalanzila.
Amesema kuwa kwa sasa wanafanya mazungumzo na shirika la Innovation of Africa ili kusaidia kuchimba kisima cha maji katika eneo hilo.