Dodoma FM

Vijana walindwe matumizi ya dawa za kulevya ili kufikia ndoto zao

12 November 2025, 1:13 pm

Picha ni dawa za kulevya aina mbalimbali ambazo hutumiwa hususani na vijana .Picha na DCEA.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kukevya (DCEA) imesema kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu ndio linaloongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya ikiwemo uchepushwaji wa kemilaki bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.

Na Seleman Kodima.
Imeelezwa kuwa ili vijana waweze kufikia malengo yao ya maisha, ni muhimu wakalindwa dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, ambazo zimeendelea kuwa tishio kwa afya na maendeleo yao.

Katika mahojiano maalum na, Anna Tengia kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kanda ya kati, amesema mamlaka hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vijana wanakuwa salama dhidi ya vishawishi vya matumizi ya dawa hizo hatari.