Dodoma FM

Daladala zipakie na kushusha abiria katika vituo rasmi

12 November 2025, 12:46 pm

Ushushaji na upakiaji wa abiria katika vituo visivyo rasmi unaweza kusababisha ajari zisizo za lazima.Picha na AI.

Abiria pia wanapaswa kuwa waelewa na waache kuomba kushushwa vituo visivyo rasmi.

Na Farashuu Abdallah.
Madereva wa daladala wametakiwa kupakia na kushusha abiria katika vituo rasmi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.

Hayo yamesemwa na Afisa Mfawidhi kutoka mamlaka ya usafirishaji Mkoa wa Dodoma Ezekiel Emmanuel wakati akizungumza na Dodoma Fm amesema ushushaji na upakiaji wa abiria katika vituo visivyo rasmi unaweza kusababisha ajari zisizo za lazima na kuleta changamoto kwa watembea kwa miguu pindi wanapohitaji kuvuka barabara.

Sauti ya Ezekiel Emmanuel .

Kwa upande wao madereva wametoa ombi kwa abiria kuwa waelewa na kuacha tabia ya kuomba kushushwa vituo visivyo rasmi.

Sauti za madereva.