Dodoma FM
Dodoma FM
10 November 2025, 4:00 pm

Mtu mwenye magonjwa yasiyoambukiza anaweza pia kuathiriwa na magonjwa ya kuambukiza.
Na Seleman Kodima.
Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza mkoani Dodoma, Dkt. Missana Yango, amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya kinywa na ubongo, akibainisha kuwa matatizo ya kinywa yanaweza kuathiri mfumo wa fahamu na kuhatarisha afya ya mtu kwa ujumla.
Akizungumza leo, Dkt. Yango amesema mtu mwenye magonjwa yasiyoambukiza anaweza pia kuathiriwa na magonjwa ya kuambukiza, na vivyo hivyo, hali inayodhihirisha umuhimu wa usimamizi wa afya kwa ujumla.
Ameeleza kuwa matatizo ya meno kama kuoza au kutoboka yanaweza kuruhusu vimelea vya magonjwa kuingia ndani ya jino, na kusababisha maambukizi makubwa yanayoweza kusambaa hadi kwenye fizi, ubongo, na hata uti wa mgongo.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2025 kutoka Wizara ya Afya imebainisha kuwa Zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanakabiliwa na changamoto za afya ya kinywa na meno.
Huku Asilimia 35 ya wagonjwa wanaofika hospitalini kwa matatizo ya meno huwa tayari wamepata maambukizi yanayohitaji matibabu ya dharura