Dodoma FM
Dodoma FM
10 November 2025, 12:46 pm

Kupitia shughuli ya ukusanyaji wa plastiki, kazi hii imekuwa chanzo cha ajira na kipato cha familia.
Na Lilian Leopold.
Kile ambacho wengi hukiona kama taka, kwa wengine ni njia ya kujipatia ridhiki, jijini Dodoma shughuli ya ukusanyaji wa plastiki imekuwa mkombozi kwa baadhi ya familia zinazotegemea kipato chake kutokana na plastiki hizo.
Kupitia shughuli ya ukusanyaji wa plastiki, kazi hii imekuwa chanzo cha ajira na kipato cha familia, licha ya changamoto na mitazamo hasi kutoka katika jamii. Leo nakukutanisha na Mzee Julias Talibo, mkazi wa Mnada wa zamani, jijini Dodoma anayejishughulisha na ukotoji wa plastikia ambaye amesema shughuli hii imekuwa ikimsaidia kuendesha maisha yake.