Dodoma FM

Migogoro ya familia inavyoathiri malezi ya watoto

7 November 2025, 4:34 pm

Miongoni mwa athari zinazoweza kutokea ni pamoja na kuathirika kisaikolojia kwa watoto.Picha na Birmiss.

jamii imetakiwa kuacha migogoro  na kuzingatia maslahi ya watoto katika familia.

Na Anwary Shaban.

Imeelezwa kuwa migogoro na ugomvi kati ya baba na mama ndani ya familia ni miongoni mwa vichocheo vinavyochangia katika malezi mabaya ya watoto.

Kauli hiyo imetolewa na Fatuma Kibasa kutoka Taasisiya Action For Community Care (ACC) iliyopo jijini Dodoma,wakati akizungumza na Taswira ya Habari ambapo amesema miongoni mwa athari zinazoweza kutokea ni pamoja na kuathirika kisaikolojia kwa watoto.

Sauti ya Fatuma Kibasa

Taswira ya Habari imefika mtaani na kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Dodoma ambapo wananchi hao wamesema kuwa watoto wanaoshuhudia ugomvi wa wazazi wao mara kwa mara huathirika kisaikolojia.

Sauti za wananchi.

Bi. Fatuma Kibasa amehitimisha kwa kutoa wito kwa jamii kuacha migogoro  na kuzingatia maslahi ya watoto katika familia, ili kujenga jamii yenye upendo na uwiano bora wa kifamilia.

Sauti ya Bi. Fatuma Kibasa.