Dodoma FM

Wakandarasi watakiwa kuharakisha ujenzi soko la Majengo

7 November 2025, 2:41 pm

Picha ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule akiongea wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa soko hilo.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Ukarabati wa soko hilo unatekelezwa kupitia mradi wa Tactics ambapo takribani wafanyabiashara 1,795 watanufaika na soko hili.

Na Lilian Leopold.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wakandarasi wanaokarabati soko la Majengo jijini Dodoma kuhakikisha mradio huo unakamilika kwa wakati ili kuondoa msongamano kwa wafanyabiashara.

Katika ziara iliyofanyika Novemba 06, 2025 Mkuu wa mkoa akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri katika kukagua maendeleo ya ukarabati wa soko hilo Mhe. Senyamule amesema lengo la kuboresha soko hilo ni kukidhi mahitaji ya wakazi wa jiji hilo na kuendelea kukuza uchumi wa jiji.

Sauti ya Mh. Senyamule.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri amesema soko hilo litahusisha uwepo wa CCTV kamera, jengo la wakina mama kwa ajili ya kunyonyesha na kituo cha polisi.

Sauti ya Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri
Picha ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri katika ukaguzi wa soko.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Happiness Mgalula ni Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Azhar Construction amesema licha ya changamoto zilizokuwepo hapo mwanzo lakini kwa sasa mradi huo unaendelea vizuri na wamejipanga kuukamilisha kwa wakati.

Sauti ya Happiness Mgalula

Naye Mwenyekiti wa soko hilo Godson Rugazama ameeleza kuvutiwa na ubunifu uliofanywa na halmashauri katika kuhakikisha soko hilo linakuwa bora na la kisasa.

Sauti ya Godson Rugazama