Dodoma FM
Dodoma FM
6 November 2025, 3:47 pm

Serikali imedhamiria kubadili matumizi kutoka kwenye kuni, mkaa na nishati zisizosafi, kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo serikali imesema inategemea ifikapo mwaka 2034 angalau takriban 80% ya kaya za Tanzania zitakuwa zinatumia nishati safi ya kupikia.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Chanhumba kata ya Handali wilaya ya Chamwino jijini Dodoma wameiomba serikali kuwakumbuka katika mpango wa matumizi safi ya nishati ili kuwaepusha na matumizi ya kuni na mkaa.
Wananchi hao wamebainisha hayo wakati wakiongea na Taswira ya habari ya Dodoma Fm, ambapo wamesema utumiaji wa kuni na mkaa umekuwa ukiwaathiri kiafya, hivyo ili kuondokana na changamoto hiyo wameiomba serikali kuwaingiza kwenye mpango wa maalum wa kupata nishati safi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Chanhumba Bw.Amosi Lusiji amesema hapo awali mradi huo uliishia katika kata jirani ya Mvumi na wao kushindwa kunufaika na mpango huo