Dodoma FM

Wazazi watakiwa kufanya maandalizi ya shule mapema kwa watoto

6 November 2025, 2:59 pm

Maandalizi mazuri yatawasaidia watoto kuepuka kukaa muda mrefu mitaani na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.Picha na AI.

Wazazi na walezi wanapaswa kutambua kuwa elimu ni muhimu kwa mtoto, kwani itamsaidia katika kuwa na uwezo wa kujitambua na kupamabana na changamoto za maisha hivyo ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto anapata haki yake ya elimu.

Na Farashuu Abdallah.

Baadhi ya wananchi jijini Dodoma wametoa ushauri kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanafanya maandalizi mazuri kwa watoto wao ambao wanatarajia kujiunga na elimu ya sekondari, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba jana, Novemba 5, 2025.

Matokeo hayo yalitangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Profesa Said Ally Mohamed, ambapo wanafunzi waliomaliza darasa la saba walifanya mtihani huo kuanzia Septemba 10 mwaka huu.

Sauti za wananchi.

Wananchi hao wameongeza kuwa maandalizi mazuri yatawasaidia watoto kuepuka kukaa muda mrefu mitaani na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Sauti za wananchi.