Dodoma FM
Dodoma FM
5 November 2025, 4:17 pm

Aidha Mtahu ameshauri vijana kujituma katika umri wao kwani wakati huo hukutana na watu wengi ambao wangeweza kuwasaidia kutokana na nguvu kazi waliyo kuwanayo.
Na Farashuu Abdalah.
Vijana wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza hapo baadae ikiwemo tatizo la Afya ya akili .
Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii Mtahu Mtahu wakati akizungumza na Dodoma Fm amesema ni vema vijana wakatumia muda wao vizuri kwa kujishughulisha na kazi mbalimbali katika jamii ili kujijengea kesho iliyo bora.
Pia ameshauri jamii kuzingatia malezi bora kwa Watoto kwa kuwalea kwenye mazingira ya kujishughulisha na kazi za nyumbani ili kujenga Taifa lililo imara.
Nao baadhi ya Wananchi wakiwemo vijana wame wahimiza vijana wenzao kufanya kazi kwa bidii ili kujiepusha na tabia zisizofaa.