Dodoma FM
Dodoma FM
5 November 2025, 3:37 pm

Wazazi wana jukumu la kuwapeleka watoto wao kuhudhuria madarasa ya dini ili kujenga jamii yenye hofu ya Mungu.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa kukosekana kwa maadili ya kidini kwa watoto na vijana kunaweza kuhatarisha usalama wa jamii na hata Taifa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Bi.Ester Nyau Msimamizi wa Jumuiya ya wazazi katika kikao cha wananchi kilichofanyika Novemba 04 katika kijiji cha Mchito Kata ya Msisi jijini Dodoma.
Bi. Nyau amesema malezi ya dini yanaweza kuwa njia bora na sahihi kwa mtoto, kwani kupitia misingi ya dini itamfanya mtoto kukua katika hofu ya Mungu.
Nao baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mchito wamesema wazazi wana jukumu la kuwapeleka watoto wao kuhudhuria madarasa ya dini ili kujenga jamii yenye hofu ya Mungu na maadili mema.