Dodoma FM
Dodoma FM
4 November 2025, 3:00 pm

Hali imeendelea kuimarika katika jiji la Dodoma na wananchi wameendelea na shughuli zao kama kawaida huku huduma za usafiri zikirejea , maduka yaliyo kuwa yamefungwa yakifunguliwa.
Na Mariam Kasawa.
Baada ya serikali hapo jana kuruhusu shughuli za kijamii katika maeneo mbalimbali ziendeleee hapa nchini.
Dodoma fm imezungumza na Baadhi ya wenyeviti wa mitaa katika jiji la Dodoma Mwenyekiti wa Mtaa wa Fatina kata ya Majengo Bi Maua Mbaruku ambapo amesema katika mtaa wake shughuli na huduma mbalimbali tayari zimerejea huku hali ya usalama ikiendelea kuimarika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Karume kata ya Mnadani bwana Matwiga Kiatya amesema wakazi wa mtaa huo wameendelea na shughuli zao huku akiwataka wananchi kuendelea kudumisha amani na kuzingatia sheria.
Nae Afisa bishara wa soko la machinga Jijini Dodoma Mbwana Hassan amesema hali ya usalama katika soko hilo imeimarika hivyo wananchi wanaweza kufika katika soko hilo na kujipatia huduma mbalimbali .