Dodoma FM
Dodoma FM
27 October 2025, 3:40 pm

Wameiomba Serikali kupeleka wataalamu wa masuala ya kijinsia kutoa elimu kwa wanandoa, pamoja na wataalamu wa ardhi, ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Mpwayungu, jijini Dodoma, wametakiwa kuachana na migogoro ya ardhi na migogoro ya ndoa, ambayo imekuwa chanzo cha chuki na migongano ndani ya jamii.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Bw. Festo Manjechi, ambaye amesema kuwa migogoro hiyo inakwamisha amani na maendeleo ya kijiji.
Ametumia fursa hiyo pia kuiomba serikali kupeleka wataalamu wa masuala ya kijinsia kutoa elimu kwa wanandoa, pamoja na wataalamu wa ardhi, ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara.
Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mpwayungu wamesema kuwa uwepo wa migogoro hiyo unawaathiri moja kwa moja, hivyo wanaziomba mamlaka husika kutoa elimu kwa wananchi ili kuleta amani na kupunguza migongano.