Dodoma FM
Dodoma FM
23 October 2025, 4:06 pm

Changamoto hiyo imekuwa ikiathiri shughuli za wananchi hao kutokana na maji hayo kudumu kwa muda bila ya kupungua.
Na Victor Chigwada.
Kuelekea katika msimu wa masika, wananchi wa kijiji cha Majeleko Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wameonyesha kuwa na hofu kutokana na mto Kinyasungwi kujaa maji na kukata mawasiliano.
Changamoto hiyo imekuwa ikiathiri shughuli za wananchi hao kutokana na maji hayo kudumu kwa muda bila ya kupungua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Majeleko Ndg.Charlesi Milangasi amesema kukosekana kwa daraja katika mto Kinyasungwi kumekuwa na atari kubwa hasa kwa wanafunzi kutokana na kulazimika kukaa nyumbani na kusubiri maji kupungua.
Nao baadhi ya wanafunzi kutoka Kijiji jirani cha Chinangali wameeleza namna ambavyo huwaathiri kimasomo kutokana na mto huo kujaa maji.