Dodoma FM
Dodoma FM
22 October 2025, 3:20 pm

Huduma hizo za kibingwa zinatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali za rufaa, sambamba na kuinua kiwango cha utoaji wa huduma za afya katikajamii.
Na Lilian Leopold.
Wananchi Mtaa wa Ilazo na maeneo ya jirani Jijini Dodoma wametakiwa kutumia fursa kupata matibabu ya kibingwa yanayotolewa katika kituo cha afya Ilazo.
Wito huo umetolewa na Daktari kutoka Kituo cha Afya Ilazo, Stevene Adam Chikoti ambapo amesema kuwa huduma za kibingwa hizo zinahusisha tiba za magonjwa ya ndani, magonjwa ya akinamama, upasuaji na magonjwa ya watoto, hatua inayolenga kuboresha afya za wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake, Hezron Kalinga,AfisaTabibuwaKituo cha Afya Ilazo, amesema utoaji wa huduma hizo umeanza ambapo hadi sasa wagonjwa 12 wa magonjwa ya ndani wamekwishahudumiwa.