Dodoma FM

Pambano la ngumi Kibaigwa rasmi kufanyika Oktoba 25

21 October 2025, 1:03 pm

Picha ni baadhi ya mabondia watakaoshiriki katika pambano la ngumi Kibaigwa wakiwa katika mazoezi. Picha na Hamis Makila.

Pambano hilo litashirikisha mabondia 25 kutoka maeneo ya Tanzania, huku pambano kuu likiwa kati ya Anthony Boiko na George Dimoso.

Na Hamis Makila.

Pambano la ngumi lililopangwa kufanyika Oktoba 18 katika Uwanja wa Amani, Kibaigwa rasmi kufanyika Oktoba 25, hii ni kutokana na baadhi ya mabondia kutokupimwa afya zao.

Yuko Kiyando, Mkurugenzi wa Kikundi cha Ngumi cha Wizard Promotion Fitness,amesema hadi sasa mabondia wote wameshafanyiwa vipimo vya afya, na maandalizi yanaendelea kikamilifu kuelekea pambano hilo kubwa.

Sauti ya Yuko Kiyando.

Picha ni Seif Kalulu ambaye ni kocha wa pambano.

Kwa upande wake kocha wa pambano hilo, Seif Kalulu amesema maandalizi yanaendelea vizuri na ana imani mabondia wote watatoa mapambano ya kuvutia.

Sauti ya Seif Kalulu.

Nao baadhi ya mabondia wamesema kupitia mazoezi makali na mafunzo ya kikundi, wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na wapinzani wao.

Sauti za mabondia.