Dodoma FM

Yanga na Prisons kukutana uwanja wa Jamhuri Dodoma

21 October 2025, 12:00 pm

Picha ni Uwanja wa Jamhuri utakapochezwa mchezo kati ya Yanga Sc na Tanzania Prisons Novemba 01. Picha na Hamis Makila.

Uamuzi wa kuhamishia mchezo huo katika Uwanja wa Jamhuri umetokana na taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya Uwanja wa Tanzania Prisons kutokidhi vigezo vya matumizi.

Na Hamis Makila.

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga SC na Tanzania Prisons, uliopangwa kufanyika tarehe 1 Novemba, utafanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kufuatia Uwanja wa Tanzania Prisons kufungiwa.

Akifanya mahojiano na Dodoma FM katika Uwanja wa Jamhuri, Meneja wa uwanja huo Hussein Mhando amesema maandalizi yote yamekamilika ili kuhakikisha mechi zote zilizopangwa kuchezwa hapo zinakwenda vizuri.

Picha ni Meneja wa uwanja wa Jamhuri Hussein Mhando akizungumza na Dodoma FM .

Amesema tarehe 22 Oktoba timu ya Dodoma Jiji itacheza na Mtibwa Sugar, huku tarehe 25 Oktoba Dodoma Jiji ikitarajiwa kuvaana na Pamba Jiji, kabla ya mchezo mkubwa kati ya Yanga SC na Tanzania Prisons kufanyika mwanzoni mwa Novemba.

Mahojiano kati ya Hamis Makila na Hussein Mhando.