Dodoma FM

Chifu Yasin asisitiza amani kuelekea Uchaguzi

20 October 2025, 5:36 pm

Picha ni Kiongozi wa Machifu wa Mkoa wa Dodoma, Chief Yasin Bilinji. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Bilinji, amesema hakuna haja ya kuvunja amani ya taifa ikiwa zoezi la upigaji wa kura ni haki ya msingi kwa kila mwananchi.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kudumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu.

Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa machifu wa mkoa wa Dodoma  Chief Yasin Bilinji katika hafla maalum ya kuombea Taifa iliyofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki.

Chief Bilinji amemtaka kila mtu kutambua kuwa Tanzania ni moja na hakuna nyingine hivyo ni vyema kushiriki zoezi la kupiga kura Kwa amani.

Sauti ya Yasin Bilinji.

Nao baadhi ya wadau wakiwemo wawakilishi asasi mbalimbali, wameitaka Jamii kuhakikisha amani inakuwepo ili kulinda nchi dhidi ya machafuko.

Sauti za wadau.