Dodoma FM
Dodoma FM
20 October 2025, 5:16 pm

Wakazi wa Kijiji cha Chanhumba wamesema licha ya jitihada zao za kulima, mazao yao yalikauka kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha. Picha na Dodoma FM.
Wakazi wakijiji hicho wameiomba serikali kuwasaidia kupata mahindi kwa bei nafuu ili kukabiliana na hali ya njaa inayowakabili.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji cha Chanhumba wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula.
Wakizungumza na Dodoma FM wakazi hao wameeleza kuwa pamoja na jitihada walizofanya za kulima hawakuweza kupata mavuno kutokana na kukosa mvua za kujitosheleza.
Wameeleza kuwa kwa sasa wanalazimika kula mlo mmoja au kukosa kabisa jambo linaloathiri watoto kitaaluma.
Wakazi hao wameiomba serikali kuwasaidia mahindi ya bei nafuu kupeleka mahindi ya bei nafuu
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chanhumba Ndg. Amosi Lusiji amekiri uwepo wa changamoto ya njaa kijijini hapo ambapo amebainisha kuwa inaathiri shughuli za maendeleo kwa ujumla.