Dodoma FM

Wachimbaji wadogo watakiwa kuchukua tahadhari migodini

17 October 2025, 3:39 pm

Wachimbaji wadogo wa madini wametakiwa kutumia vifaa vya kinga migodini ili kuepuka madhara ya kemikali yanayoweza kuathiri afya zao. Picha na Blogers.

Kwa kuzingatia matumizi ya vifaa sahihi wakati wa uchimbaji wa madini wataweza kuepukana na athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na kemikali zinazotumika migodini.

Na Victor Chigwada.

Jamii ya wachimbaji wadogo wa madini imeaswa kuchukua tahadhari na kuhakikisha wanatumia vifaa vya kinga ili kulinda afya zao wanapofanya kazi migodini.

Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Kemikali katika Migodi ya Nholi, Ndg. Renatusi Mateso wakati akizungumza na wachimbaji hao.

Amesisitiza kuwa kukosekana kwa vifaa vya kinga kunaweza kupelekea madhara makubwa, ambayo mara nyingi hayaonekani mara moja.

Sauti ya Renatusi Mateso.

Nao baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wa eneo la Mgodi wa Nholi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya kemikali, ili kuelewa madhara yanayoweza kutokea kutokana na kemikali zinazotumika kwenye machimbo.

Sauti za wachimbaji.