Dodoma FM

Ukosefu wa huduma za afya karibu changamoto kwa wajawazito

17 October 2025, 10:48 am

Ukosefu wa huduma za afya kijiji cha Ilangali umetajwa kuwa changamoto hasa kwa mama wajawazito. Picha na Dodoma FM.

Ukosefu wa huduma za afya maeneo ya karibu unawafanya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo jambo ambalo ni hatari kwa wanwake wajawazito.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa vitongoji vya Maondo na Matembe, vilivyopo katika Kijiji cha Ilangali, tarafa ya Mpwayungu, wameiomba serikali kusogeza huduma za afya karibu na maeneo yao ili kuepuka adha ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu.

Wakifanya mahojiano na Dodoma FM wananchi wamesema changamoto hiyo imekuwa ikisababisha madhara makubwa hasa kwa akinamama wajawazito, ambao hulazimika kutembea kwa muda mrefu kufuata huduma za afya, hali inayoweza kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilangali, Ndugu Anania Ngodingo, amekiri kuwepo kwa changamoto ya umbali kwa wakazi wa vitongoji hivyo, akisema mara nyingi hulazimika kutembea kwa miguu kutokana na ukosefu wa usafiri wa uhakika.

Sauti ya Anania Ngodingo.

Aidha, Ngodingo ameongeza kuwa changamoto hiyo imewahi kuwakumba pia wakazi wa kitongoji cha Mafulungu, ambao walijitahidi kujenga zahanati kwa nguvu zao, ingawa ujenzi huo bado haujakamilika kutokana na ukosefu wa rasilimali.

Sauti ya Anania Ngodingo.